25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Ahukumiwa miaka mitatu jela kwa kukutwa na bangi

AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es salaam imemhukumu jela miaka mitatu Mohamed Mwinchuya (47) maarufu Babe kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Akisoma hukumu hivyo leo mahakamani hapo, Hakimu Joyce Mushi amesema kutokana na mshtakiwa kukiri kukutwa na dawa hizo kwa mujibu wa sheria atatakiwa kutoa faini ya Sh millioni 1 au kwenda jela miaka mitatu.

Katika kesi ya msingi mshtakiwa anadaiwa kuwa Machi 1 mwaka huu eneo la Boko Chama Wilaya ya Kinondoni alikutwa na dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kilo 1.09.

Hata hivyo Mshtakiwa amekiri kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya, na kuomba Mahakama impunguzie adhabu kutokana na kutegemewa na familia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles