29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Makonda arejesha tabasamu la Pasco Cassian

NA BRIGHITER MASAKI.

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametembelewa na msanii wa nyimbo za Injiri nchini Pasco Cassian kwa lengo la kutoa shukrani na kathibitisha kuwa amepona tatizo la mfumo wa figo na kibofu cha mkojo tatizo lililokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu na kufanya familia yake kupoteza matumaini.

Akizungumza ofisini kwake Makonda alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kutenda miujiza yake kwa Pascal ambaye aliondoka nchini akiwa na mifuko ya kuhifadhia haja ndogo na leo hii Pascol ananitembelea akiwa anatembea mwenyewe kwa miguu na kupata haja kama ilivyokuwa zamani.

“Namshukuru Mungu kwa kumponya mtu ambaye watu baadhi ya watu walisema kuwa hawezikupona na wengine kusema hadharani kuwa pesa nilizozitoa ni sawa na kutupa kwenye shimo la chooni, lakini napenda kuwashukuru wote watu wote waliomuunga mkono kumuombea  hadi kapona, niwaombe watanzania kuwa na moyo wa upendo wakusaidia wahitaji ”anasema Makonda.

Kwa upande wake Pascol Cassian amemshukuru Makonda na kumuakikishia kuwa amepona na sasa anaweza kuendelea na shughuli zake za kutafuta kipato kama alivyokuwa awali.

Na upande wa familia na mke na watoto wake wamesema kuwa awali hao wanafamilia walikata tama kwa hali aliokuwa nayo awali lakini wamepata timaini jipya walipohakikishiwa na Makonda na kumshukuru kuwa nao bega kwa bega nao hadi amepona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles