27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Sarah wa Harmonize ashindwa kupanda mlima, abebwa mgongoni

Florence Sanawa, Mtwara

Katika hali isiyo ya kawaida, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Harmonize kutoka WCB, amejikuta akimbeba mgongoni mpenzi wake Sarah baada ya kushindwa kupanda Mlima Mkomaindo ulioko mkoani hapa.

Tukio hilo limetokea jana wakati msanii huyo akiwa mjini ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Masasi Rock Festival, lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Wakati wa kupanda mlima huo, Sarah ambaye ni raia wa Italy, alionekana kuchoka na kushindwa kuendelea ambapo katika isiyotegemewa na wengi Harmonize ambaye ni mwenyeji wa Mtwara alimbeba mgongoni na kuwaacha watu waliokuwapo hapo kuangua vicheko.

Katika tamasha hilo kunatarajiwa kufanyika mashindano mbalimbali ikiwamo kupanda jiwe mkomaindo lenye urefu wa mita 1,800.

Tamasha hilo limeanza jana na litamalizika Juni 9, mwaka huu likiwa na lengo la kutangaza utalii wa ndani ya mkoa wa Mtwara. Kaulimbiu ya Tamasha hilo ni ‘Tukutane Kileleni.’

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles