26.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Makamu wa Rais kuwafunda wasanii athari za dawa za kulevya

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Mamlaka ya Kupambana na kuzuia  Dawa za Kulevya nchini imepanga kukutana na wasanii mbalimbali ili kuwapa elimu ya madhara ya dawa za kulevya ikiwa wao ni miongoni mwa wa  waathirika wa dawa hizo kwa kutumia au kutumiwa kama wabebaji.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo kugundua kuwa wasanii ni waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya hivyo wamepanga kutoa vipeperushi vya kila aina ya dawa za kulevya vinavyoeleezea athari zake lengo ikiwa ni kufikisha taarifa kwa watu wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Kamishna  Mkuu wa mamlaka hiyo Rodgers Sianga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Februari 11, ambapo amesema wamepanga kukutana na wasanii hao Jumatano Februari 13 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Uingizwaji wa dawa nchini umepungua, tulipodhibiti nchi kavu walihamia katika njia za bahari ambapo kwa mwaka jana pekee tulikamata tani 9, 000 za dawa za kulevya zilizotaka kuingizwa nchini kwa njia ya majini na kwa nchi kavu tulikamata kilo 1, 000 za dawa kwa kushirikiana na majeshi ya majini bila hivyo hali yetu ingekuwa mbaya sana.

“ Kuhusu matumizi hatujajua yamepungua kiasi gani hivyo tunapanga mwishoni mwa mwaka huu kufanya tafiti ili tujue yamepungua kwa kiasi gani upatikanaji wake na matumzi yake kwa waathirika wa dawa ya kulevya na ndiyo sababu ya kuwaita wasanii ili watusaidie kufiklisha elimu kwa watu wengi” amesema.

Aidha Kamishna Sianga amesema wamejipanga kuhamishia nguvu katika mipaka ya Kusini ili kudhibiti uingizwaji wa dawa kutokea nchini Msumbiji kupitika katika ya mikoa ya kusini.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,263FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles