26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘Mateja’ wageukia dawa za hospitali

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Baada ya Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana ma Dawa za Kulevya nchini kudhibiti uingizwaji na upatikanaji wa dawa hizo sasa watumiaji wake wamehamia katika dawa tiba zenye asili ya kulevya zinazopatikana katika hospitali hapa nchini kama  dawa za usingizi na za kupunguza maumivu zijulikanazo kama ‘Pethidine’ .

Hayo yamesemwa na  Mkemia Mkuu wa Mamlaka hiyo Zalawi Machibya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 11, jijini Dar es Salaam ambapo amesema watu hununua dawa hizo kama tiba ila huzidisha dozi tofauti na inavyotakiwa kutumiwa na huathirika bila wao kujua na kujikuta wanahitaji kuzitumioa mara kwa mara.

Amesema wamekamata mtandao unaojihusisha na uuzaji wa dawa tiba zenye asili ya kulevya katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na watuhumiwa wamefikishwa katika vyombo vya sheria taratibu zingine zikiendelea na wengine 12 bado wanachunguzwa na watakapobainika watafikishwa katika vyombo vya sheria.

“Kuna mgonjwa tulimshuhudia akiuziwa dawa hizi za Pethidine lakini si kwa ajili ya kujitibia ambapo alikuwa anatumia chupa 15 kwa siku na kikawaida inatakiwa uitumie chupa mbili au tatu kwahiyo kesi kama hizi hizipo na katika mikoa hiyo miwili tumedhibiti na tutahamia katika mikoa mingine pia,” amesema Machibya.

Aidha Machibya amesema dawa zingine zinapotengenezwa huweza kutumika hata kwa watoto wa shule za Sekondari na Msingi ambao huzitumia hata wakiwa wakubwa na kuwapelekea kufanya vitendo viovu hivyo wamejipanga kudhibiti mitandao na kuhakikisha dawa tiba zinatumika kama ilivyokusudiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles