Makamu wa Rais asikitishwa na kasi ya uharibifu wa mazingira, mipango kubaki kwenye mafaili

0
634

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema anasikitishwa na kasi ya uharibifu wa mazingira inayofanywa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

“Tukijitathmini kama jumuiya, kwa kutumia mipango iliyoasisiwa na jumuiya hasa ule mpango wa 2003-2020, lakini utagundua kuwa nyingi kati ya nchi zetu za SADC zinakuwa na mipango mizuri za kukabiliana na changamoto za mazingira lakini inabaki kwenye mafaili,” amesema Mama Samia jijini Arusha leo Ijumaa Oktoba 25, wakati akifungua mkutano mkuu wa mawaziri wa SADC wa maliasili na utalii.

Amesema nchi za SADC zimebarikiwa kuwa na maliasili nyingi, lakini zinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwamo uchafuzi wa mazingira, uharibifu wa misitu, uharibifu wa mifumo ya maisha ya viumbe wa majini, uharibifu wa misitu, upotevu wa makazi ya wanyamapori na bioanuwai.

“Ni jambo la kusikitisha kuona kasi yetu wa uharibifu wa mazingira ni kubwa kuliko juhudi tunazofanya ili tuweze kukabiliana na changamoto hizi na kuokoa rasilimali tulizobarikiwa.

“Wote tuna wajibu wa kulinda rasilimali hizi na kuhakikisha kuwa tunaanzaa mikakati inayoendana na itifaki na mipango mikakati ya kutenga fedha na kuhakikisha kunakuwapo na wataalamu wa kutosha wa masuala ya mazingira na kuzingatia kutoa elimu ya kutosha ya kulinda na kuhifadhi rasilimali za mataifa yetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here