Na WINFRIDA NGONYANI,DAR ES SALAAM
MAJI ni uhai. Maji yanafaida nyingi katika mwili wa binadamu ikiwa tu yatatumika ipasavyo. Hapa namaanisha kuwa pendelea kutumia maji safi na salama kila wakati ili kujiepusha na magonjwa ya homa ya tumbo.
Kunywa maji kwa wingi kunasaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula mwilini, ambapo kama utakunywa maji kwa wingi mara baada ya kumaliza kula, chakula chako kitasagwa vizuri hivyo kukusaidia kupata choo laini.
Tibu tatizo la maumivu ya kichwa kwa kunywa maji mengi angalu lita 3-5 kwa siku, hakika unaweza kutuliza maumivu hayo kwa asilimia kubwa endapo tu maumivu hayo yatakuwa ni ya kawaida.
Ukinywa maji kwa wingi pia utaifanya ngozi yako kuwa nyororo na yenye mvuto kwa sababu yanasaidia kuboresha tishu za ngozi yako na kuongeza unyevunyevu kwenye ngozi.
Maji yanafaida nyingi mno katika kuboresha afya yako, na hizi ni baadhi tu ya faida hizo.