23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wataalamu: Vitamini nyingi hazifai kwa wajawazito

o-PREGNANT-WOMAN-facebook

Utafiti mpya wa wataalamu umebaini kuwa tembe za vitamin mseto zinazotolewa kwa wajawazito huwa ni kupoteza fedha bure.

Kwa kawaida, wajawazito wamekuwa wakipewa tembe zenye aina ya vitamin hata zaidi ya 20 pamoja na madini mengine.

Matokeo ya tathmini hiyo, yamechapishwa katika jarida la Drug and Therapeutics Bulletin, ambalo huwafahamisha madaktari na wauzaji dawa nchini Uingereza kuhusu tiba na udhibiti wa maradhi.

Utafiti huo umegundua kwamba vitamini mseto huwa haziwawezeshi wajawazito na watoto wao kuwa na afya bora na kwamba ni ‘gharama isiyo na maana.’

Badala yake, wataalamu hao wanapendekeza kwamba wanawake wanafaa kuangazia zaidi kumeza au kunywa vitamin zilizo kivyake ambazo kwa mfano nchini Uingereza hupatikana kwa peni kadhaa.

Wataalamu hao wanasema; vyakula vyenye afya ni muhimu.

Vitamini hizo, ambazo hupendekezwa na Shirika la Taifa la Afya Uingereza (NHS), ni vitamin B9 au kwa Kiingereza folic acid miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na vitamin D.

Wanachoshauriwa

Mama na mtoto wake wanashauriwa kuendelea kuwa na afya bora kwa kupata chakula cha kutosha chenye virutubisho.

Kupumuzika muda mrefu kila siku, kuepuka kemikali, pombe, moshi na kunywa dawa nyingi. Pia wanashauriwa kupata huduma kutoka kwa mkunga au mfanyakazi wa afya mwingine ambaye anaweza kutibu, au kusaidia kupata matibabu kwa ajili ya tatizo lolote la kiafya ambalo linaweza kujitokeza.

Kuonyeshwa upendo na huruma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles