23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA, MAKAMU WA RAIS CUBA WATETA

Na Mwandishi Maalumu

-HAVANA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba, Gladys Bejarano na kumuhakikishia ufunguzi wa ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Amesema Tanzania inayatambua na kuyathamini mahusiano mazuri ya kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi, kielimu, kiafya na kiutamaduni kati yake na Cuba, hivyo inatarajia kufungua ubalozi nchini humo ili kurahisisha utendaji wa kazi za kibalozi.

Waziri Mkuu alikutana na Gladys juzi wakati alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi nchini Cuba ambapo ziara hiyo ilikuwa na la kuimarisha  kuimarisha na kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

“Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati Tanzania na Cuba, ambayo yalikuwepo kuanzia Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere, hivyo lazima tufungue ofisi za ubalozi na tutamleta balozi wetu hapa,” alisema Majaliwa.

Pamoja na hali hiyo pia Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Cuba kwa ujenzi wa kiwanda cha dawa za kuulia vijidudu vya maralia pamoja na ufadhili wa masomo ya udaktari inaoutoa kwa wanafunzi wa Kitanzania ambao wanasoma katika vyuo mbalimbali nchini humo.

Hata hivyo aliiomba Serikali hiyo iendelee kutoa ufadhili wa masomo kwa madaktari hao hadi ngazi ya shahada ya uzamili kwa sababu Serikali ya Tanzania inawahitaji madaktari bingwa wengi kwani walioko nchini ni wachache.

Kwa upande wake, Gladys alimshukuru Waziri Mkuu kwa kufanya ziara nchini Cuba na alimuhakikishia kwamba uhusiano wa Serikali yake na Serikali ya Tanzania utaendelea kuimarishwa kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Alisema Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli inafanya jitihada kubwa za kuhakikisha uchumi wake unakua kwa kasi jambo ambalo ni tofauti na mataifa mengine. “Nawapongeza kwa hatua za kimaendeleo mnazozifanya.”

Makamu huyo wa Rais alisema Serikali ya Cuba itaendelea kushirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa Sekta za Afya, Utamaduni, Kilimo, Uchumi na Elimu. Kuhusu ombi la kuongeza ufadhili wa shahada ya uzamili kwa madaktari  alisema amelipokea na atalifanyia kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles