28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

WATU MILIONI 1 HUFARIKI KWA AJALI KILA MWAKA

Na GUSTAPHU HAULE

-PWANI

ZAIDI ya watu milioni 1.2, hufariki dunia kila mwaka duniani kutokana na ajali za barabarani.

Pia watu milioni 20 hadi milioni 50, hupata ulemavu kutokana na ajali hizo.

Takwimu hizo zimetolewa juzi na Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia kwa Mratibu wa Program ya Usalama Barabarani nchini, Mary Kessi, alipozungumza katika mafunzo ya usalama barabarani, mjini Kibaha.

Mafunzo hayo yalihusisha Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa).

Katika mazungumzo yake, Kessi alisema ajali hizo zinatokana na baadhi ya watu kutozingatia sheria za barabarani ikiwamo kushindwa kuvaa mikanda, mwendokasi, ulevi, uzembe wa kushindwa kuvaa kofia ngumu kwa madereva bodaboda pamoja na vizuizi vya watoto.

“Kutokana na hali hiyo, WHO kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwamo Tamwa, Wizara ya Afya pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani, wameanza kutekeleza mradi wa miaka mitano wa kupunguza vifo vinavyotokana na ajali za barabarani.

“Vifo vingi vinatokea zaidi katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania na inasemekana asilimia 76 ya ajali zinatokea, zinasababishwa na madereva kwa asilimia 62.

“Kutokana na hilo, ndiyo maana katika mradi huo Tanzania imepewa kipaumbele ili kuhakikisha jamii inaelimishwa zaidi juu ya matumizi sahihi ya barabarani,” alisema.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa  linaloshughulika na  masuala ya usalama barabarani liitwalo Global Road Safety, Tusa Bernad, aliiomba Serikali ihakikishe inafanya mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973 ili iweze kwenda na wakati.

“Sheria hiyo imekosa baadhi ya vipengele ikiwamo cha vizuizi vya watoto na pia inatoa adhabu ndogo hususani kwa madereva wanaosababisha ajali za barabarani,” alisema Bernad.

Wakati huo huo, Bernad alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tamwa katika kuhakikisha jamii inapata elimu juu ya matumizi  sahihi ya sheria ya usalama barabarani ili kuweza kupunguza vifo na ulemavu unaotokana na ajali hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles