24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAFANIKIO

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.

Hayo aliyasema jana, jijini Dar es Salaam, alipomwakilisha Rais Dk. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.

Kutokana na hilo, aliupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji, ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na Baraka, kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa Madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini, fursa bado zipo,” alisema Majaliwa.

Kwa upande wake, Rais wa Jumuiya ya Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Amin Lakhani, aliishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba ameahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali nchini.

Alisema mtandao wa maendeleo wa Aga Khan unatoa huduma mbalimbali, zikiwamo za afya, elimu, kilimo na kuendesha miradi katika mabara ya Afrika na Asia kwa kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili kujikwamua kiuchumi.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, aliipongeza taasisi hiyo kwa mpango wake wa upanuzi wa hospitali na kuongeza vituo 35 vya afya kutoka 15 walivyonavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles