27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Majaliwa asikitishwa wizi NSSF

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, ametembelea mradi wa nyumba unaojengwa kwa ubia kati Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kampuni ya Azimio Housing Estate Limited katika eneo la Dege Beach Kigamboni na kusema amesikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaendelea kwenye eneo hilo.

Aliwaagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na Mkurugenzi wa Mkuu Kampuni ya Azimio Housing Estate Limited, Mohammed Iqbal  wakutane na Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere   wajadiliane namna ya kudhibiti wizi na kuimarisha ulinzi.

Waziri Mkuu alitembelea eneo la mradi huo jana jioni na baada ya kufika eneo ambalo linajengwa nyumba zaidi ya  7,000, alionyesha kusikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaoendelea na kutoa maagizo kwa wahusika.

“Kuna mpango gani wa ulinzi wa mali hapa, mali zinaendelea kuibwa, tutakuja kuanza ujenzi hapa na kukuta hakuna mali hata moja. Ulinzi lazima uimarishwe pande zote mbili za mradi huu eneo la ujenzi na eneo la kuhifadhia vifaa vya ujenzi,” alisema/

Erio alimuahidi Waziri Mkuu atahakikisha anakutana na wenzake waliotajwa   kujadiliana   namna ya kuimarisha ulinzi na kutatua changamoto ya wizi wa mali unaoendelea katika eneo hilo.

Mkataba kati ya NSSF na Azimio Housing Estate Limited (AHEL) ulisainiwa mwaka 2012 na kuanzisha kampuni ya hodhi ya “Hifadhi Builders” ambako AHEL ilikuwa na asilimia 55 na NSSF asilimia 45.

Katika asilimia 55 za AHEL, asilimia 20 ni ardhi iliyotoa kwenye mradi na asilimia 35 angetakiwa kuweka fedha taslimu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles