Majaliwa aikaribisha Kampuni ya Reli Urusi kuimarisha Tazara, Reli ya Kati

0
1098
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli ya Urusi (Russian Railways Company), Alexander Misharin kabla ya mazungumzo yao jijini Sochi nchini humo, jana. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mwandishi Wetu, Urusi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameikaribisha nchini Kampuni ya Reli nchini Urusi kuwekeza nchini hususani katika sekta ya ujenzi, ufundi na mafunzo ikishirikiana na makampuni ya Watanzania.

Majaliwa amesema hayo jana wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli ya Urusi, Alexander Misharin nchini humo ambako anamwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na Urusi (Russia-Africa Summit).

Amesema Tanzania inahitaji kuimarisha usafiri wa ndani wa reli hasa katika Majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga.

“Kampuni hii yenye uwezo mkubwa wa kujenga reli mpya, kukarabati reli, kutengeneza injini za treni na mabehewa pamoja na ukarabati wake inahitajika sana nchini ili kufanikisha mpango wa Serikali wa kuimarisha reli za zamani za Tazara, Reli ya Kati na kufugua reli ya Kaskazini inayounganisha mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Kilimanjaro na Arusha. 

“Katika kipindi hiki ambacho Tanzania inajenga reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) pamoja na kufufua Reli ya Kaskazini, inaikaribisha Kampuni ya Russian Railways kwa mikono miwili ije ifanye mazungumzo rasmi na Wizara husika,” amesema Majaliwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Russia Railways, Misharin alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa kampuni yake iko tayari kushirikiana na wafanyabiashara wa Kitanzania katika kuanzisha makampuni ya pamoja ili kuipatia Tanzania tekinolojia ya masuala ya reli na kubadilishana ujuzi. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here