DC Bunda: Vyama vya siasa chagueni viongozi bora kura za maoni

0
910

Mwandishi Wetu, Bunda

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili amevitaka vyama vya siasa kupitia kura za maoni kuchagua viongozi bora ambao watawasaidia kutatua changamoto za wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wilayani Bunda, alisema kiongozi bora ni yule  anayeleta tija katika wilaya na kwamba kiongozi bora lazima aoneshe dhamira yake ya kukabiliana na changamoto mbalimbali  zinazowagusa wananchi.

“Uongozi bora ni kuhakikisha ushiriki wa wananchi unaongezeka katika kuchagua viongozi watakaowawakilisha kwenye mitaa, vitongoji na vijiji.

“Pia ili kumuunga mkono Rais  John Magufuli, ni pamoja na kuchagua kiongozi mwenye nia ya dhati na thabiti, mwenye mtazamo chanya na serikali ya awamu ya tano,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, Mkuu wa Wilaya aliwapongeza wananchi wote ambao wamejiandikisha katika orodha ya daftari la mpiga kura.

Alitoa wito kutoacha kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotegemewa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here