25.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Majaliwa ahamia Dodoma, atoa anyo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya kuonana naye itabidi amfuate Dodoma na atarudi Dar es Salaam pindi atakapoitwa na Rais Dk. John Magufuli au Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana jioni alipozungumza na viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea baada ya kuwasili ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25, mwaka huu kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu.

“Tukio hili la kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio. Tumeshatekeleza. Kama kuna waliokuwa wanafikiria kwamba halitekelezeki watambue kwamba tayari tumeshafika,” alisema Majaliwa na kuongeza:

“Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa.

“Mkakati uliopo wa kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote kuishi bila bugudha yoyote.

“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari, mwakani. Mimi nimeshatangulia na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo.”

Aliwataka watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila mmoja ajipange na akarudia wito wa Dk. Magufuli kwamba atakayegoma kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,528FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles