22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa aagiza walioiba nondo Moshi wakamatwe

Mwandishi wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah kuwasa na kuwatia mbaroni watu waliohusika na wizi wa tani tano za nondo na kisha wakatoroka.

Alitoa agizo hilo jana Alhamisi, Julai 18, alipokua akizungumza na wafanyakazi na wananchi mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Moshi, katika kata ya Ngangamfumuni, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro

Majaliwa aliyeko mkoani humo kwa ziara ya kikazi za siku nne amesema mradi huo ni maalum kwani uko miongoni mwa miradi ambayo Serikali imekuwa ikiweka utaratibu wa kupelekea fedha kwenye miradi iliyotengwa na halmashauri.

“Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni tisa za kuanzia mradi huu lakini inasikitisha kuona kwamba wakazi wa Moshi mnahujumu kwa kuiba vifaa vya ujenzi, ninazo taaarifa kuwa hapa zimeibiwa tani tano za nondo na zimeshakamatwa. Manispaa iweke utaratibu wa ulinzi ili vifaa vingine visipotee zaidi, Mkuu wa Wilaya chukua hatua ya kuwafuatilia wote waliohusika,” alisema.

Ujenzi wa stendi hiyo unatarajiwa kukamilika Januari 2021 ambapo utagharimu sh bilioni 28.8 na unafanywa na mkandarasi mkuu ambayo ni kampuni ya CRJE ya China ikishirikiana na wakandarasi wasaidizi watano.

Stendi hiyo itakuwa na ofisi, maduka, migahawa na hoteli, itakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 300 kwa siku ambayo yataingia na kutoka ambapo kati ya mabasi hayo 72 yanaweza kuegeshwa kwa wakati mmoja. Pia kutakuwa na maegesho ya ya magari binafsi 218, teksi 34 na bajaji na bodaboda 20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles