31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Maiti yaokotwa ikiwa imekatwa sehemu za siri, titi

Derick Milton, Simiyu

MWILI wa mwanamke mmoja ambaye jina lake halijatambulika anayekadiliwa kuwa na kati ya miaka 25 na 27 umekutwa ukiwa umetupwa katika nyumba chakavu huku ukiwa umekatwa sehemu za siri na titi lake la upande wa kushoto.

Tukio hilo limetokea Februari 15 huko Kijiji cha Lamadi, Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Baadhi ya mashuhuda ambao ni wakazi wa kijiji hicho, wameiambia Mtanzania Digital kuwa walikuta mwili wa manamke huyo katika jumba hilo ukiwa hauna sehemu hizo.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Tano Mwera amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na mwili wa marehemu umepelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali teule ya Mkoa wa Simiyu.

Jeshi la Polisi wilaya hiyo limesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea na maiti bado imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles