Magufuli: Dar haiwezi kufungiwa kwasababu ya corona

0
667

Anna Potinus

Rais John Magufuli amesema jiji la Dar es Salaaam haliwezi kufungiwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona kwababu asilimia 80 ya ukusanyaji wa kodi kwa nchi nzima inapatikana jijini humo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Aprili 22, Wilayani Chato mkoani Geita alipokuwa akizungumza na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu hali ya virusi hivyo nchini.

“Wapo wengine wanatoa mawazo ya kuifunga Dar es Salamaam hilo haliwezekani kwasababu karibu asilimia 80 ya ukusanyaji wa kodi kwa nchi yetu inapatikana Dar es salaam, tuendelee kuchukua hatua lakini kuifungia Dar hiyo ‘never’ na tunatakiwa tujue kuwa idadi ya watu wake ni karibu milioni sita kwahiyo uwezekano wa kuwa na wagonjwa wengi ni mkubwa ikilinganishwa na mikoa mingine,” amesema.

Aidha ameiomba Benki ya Dunia na nchi zinazoendelea kuzisamehe nchi za Afrika madeni ili fedha hizo ziweze kutumika katika kupamabana na janga hilo.

“Ugonjwa huu umekumba dunia nzima na kama tunavyofahamu uwezo wa nchi za Afrika kiuchumi hauwezi ukalingana na nchi zilizoendelea, tunaziomba nchi hizi hasa benki ya dunia badala ya kukopesha watusamehe wanayotudai.

“Kwa sisi Tanzania huwa tunalipa karibu bilioni 700 kila mwezi sasa ni wakati muafaka wa benki ya dunia ambayo imeguswa na janga hili itusamehe madeni hayo ili fedha hizo zikatumike katika kupambana na janga hili la corona,” amesema Rais Magufuli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here