25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli atua Zimbabwe

MWANDISHI WETU-Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli ametembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa (Heroes Acre) waliopigania ukombozi wa Namibia, lililopo nje kidogo ya Jiji la Windhoek nchini humo.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msingwa, ilieleza kuwa katika eneo hilo wamezikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia ambao baadhi yao walipata mafunzo katika kambi ya Kongwa nchini Tanzania.

Wengine walikuwa maofisa wa Chama cha SWAPO ambao ofisi zao zilikuwa Dar es Salaam na viongozi wakuu walioendesha mapambano wakiwa nchini hapa.

Baadhi ya mashujaa waliozikwa katika eneo hilo ni Ndimo Hamaambo, Peter Nanyemba, Theo-Ben Gurirabo na Toiro ya Toire.

Rais Magufuli aliongozana na mwenyeji wake Rais wa Namibia, Hage Geingob.

Baada ya kutembelea eneo hilo, Rais Magufuli alitembelea kiwanda cha nyama cha Kampuni ya Meatco kilichopo Windhoek.

Akiwa kiwandani hapo, alielezwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho, Jannie Breytenbach kuwa wana uwezo wa kuchinja ng’ombe 630 kwa siku, wameajiri wafanyakazi 650 na kwamba wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuanzisha viwanda vya nyama.

Rais Magufuli alisema Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo barani Afrika na ameikaribisha Meatco kuja kuwekeza nchini.

Katika ziara hiyo, ameongozana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Kabla ya kuondoka nchini Namibia kwenda Zimbabwe ambako anakwenda kufanya ziara rasmi ya kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu wa pili wa Namibia, Hifikepunye Pohamba jijini Windhoek.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles