25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Magufuli amnusuru Msigwa Segerea, amtolea faini Mil.38

Kulwa Mzee – Dar es Salaam

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa anusurika kukaa gerezani kwa adhabu ya miezi mitano baada ya Rais John Magufuli kumlipia jumla ya Sh milioni 38 kwa ajili ya kulipa faini ya Sh milioni 40.


Hatua hiyo iekuja baada ya familia ya Msigwa kuchangishana na kupata Sh milioni mbili ambazo hazitoshi kulipa faini hiyo iliyoamuliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuwatia hatiani na kuwahukumu kulipa faini na wakishindwa waende jela miezi mitano kwa kila kosa.

Kaka wa Mchungaji Msigwa, Mchungaji Beneth Msigwa amemshukuru Rais Magufuli kwa msaada huo waliokwenda kumuomba akawapa na kueleza kwamba ni ndugu kwani mjomba wao kaoa binti yake.

Pamoja na Mchungaji Msigwa na viongozi wengine wa Chadema waliohukumiwa adhabu hiyo ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, aliyekuwa Katibu Mkuu, Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu, John Mnyika, Halima Mdee, Ester Matiko, Ester Bulaya na John Heche.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles