26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Magufuli aeleza mafanikio, kutofautiana mkutano SADC

Abasi Shabani (SJMC), Dar es Salaam

Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), umehitimishwa rasmi leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais Dk. John Magufuli ameeleza jinsi walivyojadiliana kwa mafanikio huku wakati mwingine wakitofautiana.

Amesema kwa takribani siku mbili wamekutana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuiletea maendeleo jumuiya hiyo na nchi zao kwa ujumla ambao umekuwa na mafanikio makubwa.

“Mkutano wetu umefanyika katika mazingira ya utulivu, amani na upendo, ni kweli kumekuwa na kutofautiana kwenye baadhi ya hoja lakini tulifikia makubaliano.

“Sababu ya pili inayonifanya niseme tumejadili kwa mafanikio makubwa ni kutokana na ajenda zenyewe na maamuzi tuliyofikia ambayo binafsi naamini yakitekelezwa yataleta mafanikio kwa nchi wanachama na jumuiya kwa ujumla.

“Kwa pamoja tumekubaliana kuondoa viwazo vya kibiashara, ukiritimba katika maeneo ya mipakani, na rushwa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles