26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

‘Magu Chuma’ ya Simorix Jenerali yaendelea kupeta

SYDNEY, AUSTRALIA

RAPA nyota kutoka Sydney, Australia, Simorix Jenerali a.k.a The General, amewashukuru Watanzania kwa mapokezi makubwa ya video yake, Magu Chuma aliyoiachia hivi karibuni kwenye mitandao mbalimbali.

Akizungumza na MTANZANIA jana, The General alisema sababu za kuimba wimbo huo ni kutokana na sifa nyingi anazopata Rais Magufuli na raia wa Australia hivyo akiwa kama Mtanzania mzalendo anayeishi nchi hiyo akaona atumie kipaji chake kumsifu kiongozi huyo.

“Nawakilisha Diaspora wote duniani ambako wanasifu kazi za Rais Magufuli. Ngoma inaitwa Magu Chuma na inaendelea kupeta mtandaoni kutokana na ujumbe wake.

“Mimi ni kijana mzalendo siwezi kuona Rais wangu anafanya makubwa harafu nikakaa kimya, nimetumia uwezo wangu kuwasilisha kile ambacho ulimwengu unatakiwa ujue,” alisema The General maarufu kama Jenerali wa Bongo Fleva nchini Australia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles