23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MAGONJWA MAPYA 30 KUONGEZEKA KWA MWAKA

Joyce Kasiki, Dodoma

Hadi kufikia mwaka 2030 kutakuwa na magojwa mapya 30 kwa mwaka, kutoka magonjwa mapya matano hadi manane ambayo hujitokeza hivi sasa kila mwaka duniani.

Ongezeko hilo la magonjwa mapya ni kutokana na kuongezeka kwa watu duniani hususani kwa nchi zinazoendelea, utafutaji wa chakula kwa binadamu hasa katika ufugaji wa wanyama, kuongezeka kwa matumizi ya ardhi kwa sababu ya kuongezeka kwa watu, shughuli za kilimo na utafutaji madini.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Afya Moja, Profesa Japhet Kilewo wakati akitoa mada kwenye kikao kazi cha wadau wa Afya Moja kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

“Mambo yote hayo yanaongeza uwezekano wa binadamu na mnyama au mnyama pori kukaa pamoja maana mambo hayo yote hufanyikia porini,ugonjwa ukitokea kwa sasa ni rahisi kuenea kwa kasi dunia nzima kutokana na kurahisishwa kwa usafiri tofauti na zamani,” amesema Profesa Kilewo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu Faustine Kamuzora akifungua kikao kazi hicho alisema hali ya mazingira siyo nzuri kutokana na wanyama kuhama hama ambapo huhama na magonjwa yao na kuyasambaza kwa binadamu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles