24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 25, 2022

TOCHI ZA TRAFIKI PWANI ZAHAKIKIWA WAKALA WA VIPIMO

Na Veronika Romwald, Pwani    |  


WAKALA wa Vipimo Tanzania  (WMA)  umekagua vifaa vya kubidhiti mwendo maarufu kama tochi zinazotumiwa na Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, kuhakiki usahihi wa vipimo vyake.

WMA imefanya ukaguzi huo mapema leo katika mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani ambayo hufanyika Mei 20, kila mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi huo Mkurugenzi wa Ufundi wa WMA Tanzania, Stella Kahwa amesema hatua hiyo imelenga pia kuhakiki usalama wa vifaa hivyo katika kudhibiti mwendo.

“WMA hapo awali tulikuwa tunapima usahihi wa vipimo kama vile mizani lakini sasa tumeendelea kuongeza wigo wa kazi zetu tunapima usahihi wa vipimo vya sekta ya biashara,  afya na hadi mazingira,” amesema.

Amewahakikishia watumiaji wa barabara hususan madereva wasiwe na wasiwasi kwani usahihiwa vifaa hivyo ni wa uhakika.

“Wawe makini wanapokuwa barabarani kwa sababu akienda mwendo wowote uwe kasi ama la, kifaa hiki kinaweka taarifa zake, ukienda speed 70 ni 70 na kama ni 80 kinaonesha hivyo hivyo 80 ” amesema.

Amesema pamoja na ukaguzi wa tochi hizo katika mkoa wa Pwani,  maofisa wengine wa WMA wamefanya ukaguzi wa usahihi wa vifaa vya uchunguzi katika hospitali ya Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.

“Tunazidi kujiimarisha, WMA ni wanachama hai katika Shirika la Vipimo Duniani na tumetunukiwa tuzo ya nchi inayofanya kazi kwa uwazi, ” amesema.

Naye, Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Makao Makuu, Abel Swai amewahimiza madereva kuendelea kuzingatia na kutii sheria za usalama barabarani.

“Hiyo inasaidia mno kukabili ajali za barabarani,  sisi tunajiimarisha kwa sababu picha zinazopigwa kwa tochi hizi zinatumika kwa ushahidi mahakamani, ” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,160FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles