23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mafunzo uzalishaji nishati jadidifu kwa takataka yatolewa

AVELINE KITOMARY Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Human Dignity and Environmental Care Foundation (Hudefo) limesema kutokana na kuongezeka kwa uharibifu wa mazingira, wameamua kutoa elimu mbadala kwa matumizi ya uzalishaji nishati jadidifu kwa kutumia takataka ili kuweka mazingira katika hali ya usafi.

Akizungumza wakati wa mdahalo jana Dar es Salaam,  mwanzilishi wa shirika hilo, Sara Pina alisema kuwa wanafanya mjadala ili kusaidia jamii na kuelimisha kujua haki ya kutunza mazingira na jinsi ya kutumia mabaki  kutengeneza nishati. 

Alisema watu wanatakiwa kujifunza kutumia nishati jadidifu ya mabaki za vyakula ili kujipatia umeme wa jua na mkaa kwa kutumia chakula na kufaidika na nishati kwa kupata matumizi ya redio na runinga.

“Tuliona kuna tatizo la uelewa katika jamii haswa kwenye haki na utunzaji wa mazingira, kwa kutambua tatizo hili tukaja na suluhisho la kutoa elimu kwenye jamii ili iwe na uelewa kuhusu mazingira ambayo jamii wanaikosa.

“Tutakuwa tukifanya midahalo kila mwezi na kutoa elimu kwa kutumia taasisi binafsi na za Serikali na zisizo za Serikali, wanafunzi wa vyuo, walimu na madaktari, benki na wazee ili kujifunza kila mwezi ili kusaidia kujibu maswali mengi yaliopo kwenye jamii zetu,” alisema Pina.

Kwa upande wake, Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Samweli Kessi alisema kuwa walifanya utafiti Kilimanjaro, Mwanza, Ukerewe, Njombe Singida na Mafia ambako walibaini uwapo wa vyanzo vya uzalishaji umeme kwa njia ya upepo.

“Katika mikoa yote tuliyofanya utafiti tumegundua kuna chanzo cha uzalishaji wa umeme kwa kutumia upepo, chanzo cha kupata umeme wa sola na kutengeneza kiwango cha kuzalisha umeme na Tanzania kwa kutumia nishati ya jua, itatusaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kutunza mazingira,” alisema Kessi. 

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Godwin Lema,  alisema wamefanya mambo mengi yahusuyo mazingira kwa wanafunzi wa uzamifu kwenye nishati ya jua na mimea, hasa kuni na kutengeneza majiko sanifu ya kutumia kuni chache ambazo utatumia kwa muda mrefu na kutumia mtambo wa kuchemsha maji. 

“Wawepo watu wa kufuatilia mwisho wa tafiti hizi ni upi na una faida gani kwa wananchi, sio hivi hivi, ni lazima kutoa elimu kuhusiana na nini kinatakiwa kufanyika kwenye mazingira na kupata nishati tufanye mjadala kwa pamoja na tukatekeleze,” alisema Dk. Lema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles