25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rita yavunja rekodi usajili watoto

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM

WAKAZI wa mikoa ya Morogoro na Pwani wameendelea kujitokeza kusajili watoto wao walio na umri chini ya miaka mitano katika usajili unaoendelea kwa mikoa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Mawasiliano wa Wakala wa Usajili, Vizazi na Vifo (Rita), Jafari Malema, alisema tayari takwimu zinaonyesha kufikia lengo ndani ya kipindi kifupi ukilinganisha na matarajio ya awali ya kufikisha asilimia 100 ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Alisema tayari Mkoa wa Pwani wenye watoto 179,162 unaongoza kwa kusajili watoto wapatao 178,471 ambao ni sawa na asilimia 99.6 na kwa Mkoa wa Morogoro wenye jumla ya watoto 381,568 wamesajiliwa 310,616 sawa na asilimia 81.4.

Alizitaja halmashauri zinazoongoza kwa Mkoa wa Pwani ni Bagamoyo ambayo  imesajili watoto wote 19,102, Kibaha 11,461, Kisarawe 18,098 na Mkuranga  37,279 sawa na asilimia 100 kwa wilaya  zote.

Malema alisema kwa upande wa Morogoro, Halmashauri ya Malinyi imesajili watoto 22,878 na kufuatiwa na Mvomero 51,837 sawa na asilimia 91.4 huku halmashauri zilizobaki zikiwa zinaendelea.

“Mpango huo ulianza kutekelezwa rasmi katika mikoa hiyo miwili ambapo Desemba 6 mwaka jana ulizinduliwa kitaifa mkoani Morogoro na mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk. Augustine Mahiga na kuhudhuriwa na taasisi mbalimbali za Serikali na mashirika ya kimataifa,” alisema Malema. 

Pia alisema kuwa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, zinaonyesha Pwani na Morogoro ni miongoni mwa mikoa yenye idadi ndogo ya wananchi waliosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles