22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mafundi umeme REA mbaroni kwa kuomba rushwa

Florence Sanawa, Mtwara

Mahakama ya Wilaya ya Masasi imewatia hatiani watumishi wawili wa kampuni ya JV RADI SERVICES LTD ambayo imeingia makubaliano na Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) kwaajili ya usambazaji umeme katika vijiji mbalimbali wilayani humo. 

Akitoa hukumu hiyo leo Juni 19, Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Masasi, Batista Kashusha amesema kuwa mahakama hiyo imewatia hatiani Michael Mhagama na Masanyiwa Michael ambao ni mafundi umeme kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya Sh 150,000 kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ambapo Masanyiwa anashitakiwa kwa kosa la kupokea rushwa ya Sh 100,000 kinyume cha sheria. 

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani Juni 18 mwaka huu na kufunguliwa Shauri la jinai namba CC73/2019 na kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka wa Taasis ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Cecilia Nshiku ambapo wamekiri kutenda makosa hayo  hivyo wametiwa hatiani. 

Amesema kuwa watuhumiwa wote walihukumiwa kwenda jela Miaka miwili ama kulipa faini kiasi cha shilingi 500,000/- ambapo wote wamelipa faini hiyo. 

Awali mahakama ilielezwa kuwa kati ya Mei 27 na 28  mwaka huu mtuhumiwa Mhagama akiwa anatekeleza majukumu Katika wilaya ya Masasi aliomba rushwa ya Sh 150,000 kutoka kwa Yusuph Bushiri mkulima mkazi wa kijiji cha Mumbaka ili aweke nguzo moja ya umeme katika nyumba yake huku huyo mwananchi akiwa tayari ameshalipia Sh 27,000  Katika ofisi ya Shirika la Umeme (TANESCO) wilaya ya Masasi. 

Aidha kwa upande wa Masanyiwa inadaiwa kuwa Mei 28 mwaka huu akiwa Katika majukumu yake ya kazi alielekezwa na Mhagama kwenda kwa Bushiri kuchukua Sh 100,000 kwa njia  yake kwaajili ya kuweka nguzo moja ya umeme.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara, Stephen Mafipa amesema kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia maagizo wanayopewa ya kutoa taarifa za rushwa na kukemea vitendo hivyo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles