27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Maelfu wafurika kupata bure huduma ya afya Simiyu

Na DERICK MILTON-SIMIYU

Zaidi ya wakazi 4000 kutoka katika kata nane za Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wamejitokeza kwa wingi katika shule ya msingi Ngulyati, kwa ajili ya kupatiwa bure huduma mbalimbali za afya kutoka kwa madaktari bigwa 50.

Akielezea lengo la zoezi hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiislamu (The Islamic  Foundation), Mubaraka Said amesema kuwa wameamua kutoa bure huduma hizo kwa wananchi ikiwa ni moja ya malengo makuu ya kusaidia jamii kwa kuwaunganisha watanzania bila kujali dini wala kabila zao.

“Taasisi yetu imeamua kutoa huduma hii kwa kila jamii, hii ni moja ya malengo tuliyojiwekea ya kusaidia jamii inayotuzunguka, afya ni muhimu, tofauti zetu katika dini na kabila haziwezi kututenganisha tukashindwa kusaidiana katika mambo ya muhimu kama haya,” amesema Mubaraka.

Wananchi waliohudhuria katika zoezi hilo wametoka katika kata  za Gamboshi, Kilalo, Sakwe, Ngulyati, Mwasubuya, Kasori, Mhango na Itubukilo ambapo zipo ndani ya Wilaya ya Bariadi.

Madaktari waliohusika katika utoaji wa huduma hiyo wametoka katika Mkoa wa Mwanza, Shinyanga na Simiyu kwa ufadhiliwa wa taasisi hiyo ya Kiislamu chini ya uratibu wa kampuni ya pamba ya Allience Ginnery iliyopo Wilayani humo.

Kwa upande wake meneja wa kampuni ya Allience, Boaz Ogola, amesema wao kama wawekezaji wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali kwa jamii ikiwa ni moja ya njia ya kudumisha ushirikiano na kurejesha faida kwa jamii inayoipata huduma ya kampuni yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles