28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

DC Sikonge abaini ubadhirifu katika miradi ya afya, elimu

NA ALLAN VICENT – TABORA

MKUU wa wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora, Peresi Magiri, amebaini kuwepo kwa wizi wa malighafi na matumizi mabaya ya fedha za umma zilizotolewa na serikali ili kutekeleza miradi ya elimu na afya wilayani humo.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika leo, Mei 26

, amesema kuwa serikali imetoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo lakini amebaini kuwepo kwa dosari nyingi katika miradi hiyo.

“Kuna mambo ya ajabu yanafanyika hapa, siwezi kukubali fedha za umma zipotee hivi hivi, mkaguzi wa ndani kafanye ukaguzi wa kina kwenye miradi yote inayotekelezwa katika shule zetu ikiwemo ujenzi wa hospitali ya wilaya nataka taarifa ya fedha,” amesema Magiri

Magiri alifafanua kuwa kuna mapungufu mengi katika miradi hiyo na vifaa vilivyoletwa kwa ajili ya kazi hiyo havina ubora unaotakiwa jambo linaloonesha kuwa madiwani na watendaji hawafuatilii miradi yao.

“Madiwani wote ambao ndiyo Wenyeviti wa Kamati za Maendeleo ya Kata (WDC) nawaomba msimamie ipasavyo utekelezaji wa miradi yenu ili kuepusha hujuma zinazofanywa na baadhi ya watu, mfano wa shule ya msingi Ililwansimba ambako mifuko ya saruji 20 imeibiwa,” amesema Peresi Magiri

Aidha amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Martha Luleka na Watendaji wake kufuatilia kwa kina utekelezaji wa miradi hiyo na kuchukua hatua mara moja kwa yeyote atakayebainika kuhujumu miradi hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya amelitaka Jeshi la Polisi, kukomesha biashara ya vifaa vya ujenzi wa miradi hiyo na kuimarisha doria na kukamata gari lolote litalokutwa na shehena ya vifaa vya ujenzi visivyojulikana vilikotoka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri, Peter Nzalalila amesema wanaohujumu miradi ya wananchi ni wahujumu uchumi, hivyo hatua kali za kisheria zichukuliwe ili kukomesha vitendo hivyo.

Mkaguzi wa ndani kafanye ukaguzi wa kina kwenye miradi yote inayotekelezwa katika shule zetu ikiwemo ujenzi wa hospitali ya wilaya nataka taarifa ya fedha,

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles