30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Madudu mengine mikopo ya Halmashauri Mwanza

*Watumishi Misungwiwaliomba rushwa kwa vikundi vinvyoomba mikopo

*Halmashauri ilikopesha wanafunzi waliochini ya miaka 18

*Ni katika mikopo inayotolewa na Halmashauri nchini

Na Clara Matimo, Misungwi

IMEBAINISHWA kuwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Misungwi mkoani Mwanza idara ya maendeleo ya jamii wamekuwa wakiwaomba rushwa wanavikundi wanaofika kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa Wanawake, Vijana, Watu wenye ulemavu.

Hayo yameelezwa Mei 13, mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo juu ya mapungufu mbalimbali yaliyobainishwa na tume maalum aliyoiunda ya kuchunguza sababu za  upotevu wa fedha zinazohusu mikopo hiyo wilayani humo pamoja na kuwapa elimu watendaji wanaoratibu mikopo hiyo lengo likiwa ni kudhibiti upotevu wa fedha hizo.

Amesema tume hiyo ilibaini kuwepo kwa matumizi mabaya ya madaraka katika idara ya maendeleo ya jamii kwani ilichukua maamuzi ya kununua mashine ya kutengeneza chaki yenye thamani ya Sh milioni 13.5 bila kuwashirikisha wanakikundi kiitwacho Kazi ni Moyo kilichopo Kata ya Ukiriguru katika mchakato mzima wa manunuzi.

 Alisema  wanakikundi  hao hawakuridhia  gharama ya ununuzi wa mashine hiyo, aidha tume ilibaini kwamba kikundi hicho kilipendekeza kununua mashine  mbili zenye gharama ya Sh milioni tatu ili kibaki na fedha ya kununulia malighafi na gharama za uendeshaji  wa mradi lakini idara hiyo ilikataa na kuchukua jukumu la kwenda kuwanunulia  kutokana na kutoridhishwa na bei wanakikundi waliikataa.

“Hata hivyo tume ilifuatilia mashine hiyo na kubaini hadi sasa  imehifadhiwa katika majengo ya halmashauri hiyo,  tume imabaki na maswali kuwa iweje mashine iliyonunuliwa kwa fedha za walipa kodI ituzwe mahali pasipo kuzalisha na kuendelea kutuzwa ni hasara kubwa kwani mkopo wake hauwezi kurejeshwa pia utaratibu wa kuihamisha haukufuata sheria,”alisema na kuongeza:

“Kikundi kinachojishughulisha na uchimbaji wa madini cha Imani Ishokera kiliomba mkopo wa Sh milioni 20 kwa ajili ya ununuzi wa karasha (mashine ya kusaga mawe ya dhahabu) lakini kilipatiwa Sh milioni 16.8  kilitaka kununua mashine hiyo mkoani Shinyanga kwa gharama ya Sh 8,000,000 ili kibakize kiasia cha Sh milioni 8.8 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya biashara .

“Lakini maafisa maendeleo ya jamii w alikataa ombi hilo na kuwashawishi wanunue karasha hilo kwa muuzaji mwingine ambaye alikuwa ametafutwa na maafisa hao kwa thamani ya Sh milioni 16 aliwaambia watapunguziwa Sh milioni moja kama watakubaliana na wazo hilo hivyo watainunua kwa Sh milioni 15 walipokataa waliamriwa warudishe mkopo huo.

 “Maafisa hao waliwaamuru  wanachama wa kikundi hicho warudishe mkopo huo mara moja na kama hawatarudisha watakamatwa na watafungwa kwa sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaenda wilayani humo kwa ajili ya mwenge  wa uhuru hivyo fedha hizo zitahitajika hali hiyo ilikilazimu kiikundi hicho kurejesha fedha hizo baada ya kushindwa kufanya uzalishaji,”alieleza Mhandisi Gabriel.

Aliendelea kutaja tuhuma zingine kuwa Januari 19, 2021, Afisa Maendeleo ya Jamii anayehusika na mikopo ya Halmashauri hiyo, Willihelmina Nkunga, aliomba rushwa  ya Sh 200,000 kutoka kikundi cha Wajane Misasi ili awasaidie kupata mkopo wa Sh milioni 5,000,000 pamoja na kikundi cha Walemavu Misasi Tujijali Sh 500,000 ili kisinyang’anywe mkopo wa Sh 8, 000, 000 kilichokuwa kimekopeshwa kwa ajili ya kununua mashine ya kusaga nafaka.

“Kikundi cha tujijali kilibadili mradi na kuanza kununua nafaka badala ya kusaga nafaka kama kilivyokuwa kimeeleza kwenye andiko mradi wao baada ya maafisa maendeleo ya jamii kugundua wamebadili mradi ndipo waliombwa watoe kiasi hicho cha Sh 500,000 baada ya wanakikundi kukataa waliwataka wanakikundi kurejesha fedha zote,  walirejesha na kikundi husika kuvunjika baada ya kukosa mkopo,”alifafanua .

Aidha, kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, tume hiyo imebaini mapungufu mengine kuwa ni pamoja na marejesho kufanywa na maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata na wilaya wakati wao siyo wanufaika wa mikopo hiyo, Sh milioni 73 zimekopeshwa kwa vikundi hewa, baadhi ya vikundi kuwa na wanachama ambao ni wanafunzi wenye umri chini ya miaka 18 ambayo ni kinyume na kanuni namba 6(1) E ya sheria za mikopo hiyo.

Hata hivyo, Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Pendo Naftari, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo na Mhandisi Gabriel, alikana ambapo kiongozi huyo wa mkoa aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza ianze kuchukua hatua kwa watumishi wote wa umma waliohusika na ubadhilifu huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles