28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Madalali wakamata magari wamchefua Makalla

Na Brighiter Masaki

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amekasirishwa na utaratibu usiofaa wa ukamataji  magari kwenye maegesho yasiyo rasmi.

Akizungumza wakati  wa uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Utawala la Manispaa ya Ubungo, Makalla, ameipongeza manispaa hiyo kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na kuwataka watumishi kutoa huduma bora kwa wananchi.

Makalla ameelekeza kuitishwa kikao cha dharura baina yake, Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA ili kupatia ufumbuzi, Makalla amefikia hatua hiyo baada ya kupokea Malalamiko mengi ya Wananchi.

“Wananchi wanalalamika  juu ya utaratibu mbovu unaotumika na  kama kiongozi siwezi kuruhusu jambo hilo liendelee.

“Baadhi ya vijana wanaofanya kazi hiyo wamekosa weledi na busara na wengi wao wamekuwa wakivizia mtu afanye kosa ili wamuadhibu badala ya kutoa elimu ili makosa yasifanyike.” amesema Makalla

Hata hivyo Makalla ameipongeza manispaa hiyo kwa ukusanyaji mapato hali iliyosababisha  waanze kutekeleza miradi kwa fedha za ndani na pia kutumia Force Akaunti kukamilisha miradi iliyokuwa ikisuasua ikiwemo jengo hilo la utawala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles