27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai apigilia msumari tozo miamala ya simu

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amepigilia msumari katika  tozo ya miamala ya simu  akidai Bunge ndio limepitisha na wale ambao wanapinga wanatakiwa kutoa mawazo mbadala nini kifanyike, huku akisisitiza lengo ni ifikapo 2025 Tanzania liwe Taifa tofauti kimaendeleo.

Hatua hiyo imekuja kutokana na baadhi ya wananchi kulalamikia tozo kubwa katika miamala ya simu.

Akizungumza leo,Julai 23,2021,katika  kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,Spika Ndugai,amesema wao kama Bunge ndio wameamua kuwepo tozo za miamala ya simu kwa sababu fedha zitakakazopatikana zitaenda katika mfuko maalum ambao  utawasaidia  wananchi.

“Tumepitisha sisi tukatunga sheria sisi, tunataka kuliona hilo,sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofauti,CCM hoyee,nimemaliza,”amesema Spika Ndugai.

Akizungumzia kuhusu Mkoa wa Dodoma aliwataka watendaji wa mkoa wa Dodoma kujitathimini katika utekelezaji wa majukumu yao kwani serikali imekuwa ikitimiza wajibu wake kwa kuleta fedha kwa wakati lakini tatizo lipo kwa watendaji.

“Hapa nitolee mfano Mkuu wa Mkoa wa Antony Mtaka aliyetoka Simuyu, kule alifanya kazi nzuri, hivyo hapa akishindwa kufanya vizuri tujue kabisa tatizo lipo kwetu,”amesisitiza Ndugai.

Kwa upande wake, Mtaka amebainisha vipaumbele vinne ambavyo atavisimamia katika mkoa wa Dodoma.

Mtaka alivitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na elimu, migogoro ya ardhi, kilimo na ufugaji wenye tija na huduma bora za sekta za afya,huku akitangaza alizeti kuwa zao la biashara katika mkoa huo.

Akizungumzia lengo la kikao hicho mkuu huyo wa mkoa amesema  ni kwenda pamoja kama timu katika kutekeleza mambo yanayohusu maendeleo.

“Nawasii tuwe na lugha ya pamoja yapo Mambo mazuri wenzetu wameyafanya hivyo lazima tuyaendeleze, sisi Dodoma tunautofauti tunabeba haiba ya makao makuu ya nchi, hivyo ni lazima tuwe na matarajio makubwa,”amesema

Kuhusu kiwango cha elimu Mkoa wa Dodoma, amesema kipo katika hali mbaya kwa ngazi zote ikiwemo mitihani ya ‘mock’kwa mkoa haujafanya vizuri hivyo zinahitajika jitihada za ziada kuhakikisha wanafanya vizuri katika sekta ya elimu na kuondokana na aibu iliyopo.

Pia amezitaka  Halmashauri zote nane za mkoa huo, kuwa na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitauingizia mkoa fedha za kutosha kuendesha miradi mbalimbali.

Amesema Jiji la Dodoma lilikusanya sh bilioni 70 kutokana na mauzo ya viwanja sasa wapo kiwango cha sh bilioni 30 hivyo lazima watafute vyanzo vipya vya mapato na anatamani kuona ubunifu katika suala hilo.

Sambamba na hilo amesema anatamani kuona kaya zikipanda miti mingi kwa ajili ya utunzaji wa mazingira pamoja na kuweka mipango mizuri katika mkoa.

“Wapo watumishi waongo na wachonganishi siwapendi, watu wanachonganisha watu, hasa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, tumekutanishwa na kazi tufanye kazi tuheshimiane kiongozi haongozwi,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles