26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mabondia wapima uzito, Oscar atinga kama mwanafunzi

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Zaidi ya mabondia 10 wa ngumi za kulipwa wamepima uzito leo Desemba 25,2023 tayari kwa pambano lao Usiku wa Mabingwa, litakalopigwa kesho Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Kila bondia alifika eneo la kupima uzito viwanja vya Mpakani Mabibo kwa mtindo wake na mashabiki, huku Oscar Richard akitinga akiwa na nguo za shule ya msingi akiongozana na wanafunzi kibao.

Akizungumzia staili yake hiyo, amesema lengo ni kutaka watu wafahamu kuwa shule kuna vipaji vingi vya mchezo huo na vinahitaji sapoti.

“Nimevaa hivi kuwakilisha wanafunzi wenye vipaji, ambao wapo shuleni na wanahitaji kusapotiwa ili kufukia malengo yao,” amesema Oscar.

Bondia huyo kutoka Nacozzy atapanda ulingoni kupigana na Msauzi, Sabelo Ngebinyana, huku pambano kubwa likiwa kati ya Twaha Kiduku na Mganda Mohammed Sebyala.

Mabondia wengine watakaozichapa kesho ni Saidi Faraji maarufu Kichwa Kisicho na Ubongo dhidi ya Richard Mkude, Joseph Maigwisa atapigana na Jacob Maganga, Ally Ngwando na Khalid Kalama, Tampela Maurusi na Waziri Magombana, Jesca Mfinanga dhidi ya Sara Alex.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles