31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Mabingwa wa ndondi ulingoni Des 26, Kiduku ndani

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Wakali wa ndondi kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajia kuzichapa katika Usiku wa Mabingwa, huku bondia Twaha Kiduku akitarajiwa kuvaana na Mganda Mohammed Sebyala Desemba 26, 2023 kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Zaidi ya mabondia 20 wa ngumi za kulipwa wanatarajiwa kupanda ulingoni siku hiyo ambapo leo Desemba Mosi  baadhi yao akiwamo Kiduku wamesaini  mkataba na muandaaji wa mapambano hayo, kampuni ya Peaktime Sports Agency.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Dar es Salaam, Mratibu wa matukio kutoka kampuni hiyo, Bakari Khatibu amesema  siku hiyo watakuwa wanaadhimisha miaka mitano ya Usiku wa Mabingwa, pia  ni sherehe ya kutambua mchango wa mabondia waliofanya vizuri.

“Huwa mwaka mzima tunakuwa tuko bize tunafanya matukio mbalimbali ya ngumi lakini kubwa lao ndio hili linalohitimisha mwaka ni Usiku wa Mabingwa ambayo hufanyika kila mwaka siku ya Boxing Day.

“Hii ni sherehe ya kutambua mchango wa mabondia ambao tumefanya nao kazi na waliofanya kazi na mapromota wengine lakini kwa mwaka 2023 wamefanya mema katika mchezo wa ngumi,” ameeleza Khatibu.

Naye bondia Kiduku   ameishukuru Peaktime kumuandalia pambano hilo baada ya kupoteza mechi yake ya mwisho aliyopigana na bondia kutoka Afrika Kusini na kusema kipindi hiki hatafanya makosa lazima ushindi ubaki nyumbani.

“Namshukuru Meja Semunyu kwa kunipa pambano hili, nimelipokea kwa hamu. Niwaambie tu yule Msauzi atawaponza wengi, amemkanyaga nyoka mkia,” amesema Kiduku.

Bondia Mkongwe Fransic Miyeyuso  ambaye anapigana na Saidi  Bwanga, ametamba kuwa yeye bado yuko vizuri ndiyo sababu mabondia wachanga wanamkimbilia hivyo ataonyesha mchezo mzuri.

“Mimi ni bondia pekee Tanzania ambaye nacheza na mabondia wachanga, kila nayekuja  mpya lazima nimpige msasa. Wanatamani kucheza na mimi kwa sababu wananiona kama mchanga mwenzao kwa jinsi nilivyofiti,” ametamba Miyeyusho.

Kwa upande wake bondia wa kike Jesca Mfinanga anayecheza dhidi ya Sara Alex, amesema  kupewa nafasi ya kucheza siku hiyo ina maanisha ameonekana yeye ni bingwa na atamuonyesha kazi mpinzani wake.

Mabondia wengine watakaozichapa siku hiyo  Oscar Richard  dhidi ya Sabelo Ngebinyana kutoka Afrika Kusini, Maono Ally na Joseph Maigwisa, Hassan Ndonga  atatwangana na Gabriel Ochieng  wa Kenya, Ally Ngwando na John Chuwa, Charles Tondo na Nick Otieno wa Kenya, Tampera Maurus na Waziri Magombana, Saidi Tores  atavaana na Richard Mkude.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles