24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 28, 2023

Contact us: [email protected]

Maandamano makubwa Hong Kong

HONG KONG ,CHINA

WAKAZI mjini Hong Kong wamefanya maandamano mengine makubwa jana asubuhi, kuhusu mswaada tata wa kuhamishwa kwa washtakiwa kutoka eneo hilo hadi China bara.

Waandamanaji hai walikusanyika kuonyesha upinzani wao katika uhusiano wake na China bara wiki moja baada ya mzozo huo kusababisha maandamano ya watu takriban milioni moja.

Mamia ya waombolezaji pia walikuwa wakisimama katika eneo lililotengwa la kuomboleza, kuweka maua na kumuombea mwanamume mmoja aliyeanguka na kufariki juzi, baada ya kubandika bango la maandamano hayo.

Wanaharakati wa kutetea demokrasia walilitoa wito wa mgomo mkubwa kuanzia leo, Jumatatu licha ya uamuzi wa kiongozi mkuu mjini humo, Carrie Lam kusitisha kwa muda usiojulikana mjadala kuhusu muswada huo wa sheria.

Wengi wa wanaopinga mswada huo wanamtaka Lam kujiuzulu na kufutilia mbali sheria hiyo ambayo wengi wanahofia huenda ikahujumu uhuru unaofurahiwa na eneo hilo lililokuwa koloni la Uingereza na sio kwengine nchini China.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,222FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles