29.7 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Maambukizi ugonjwa wa matende, busha yapungua-Ummy Mwalimu

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema nchi imepiga hatua kubwa katika kutokomeza magonjwa ya matende na busha kwa kuokoa watu milioni 31.2 waliokuwa na hatari ya kupata maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huo.

Amesema hayo Machi 12,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kutokimeza ugonjwa huo nchini hususani Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema awali maambukizi makubwa ya ugonjwa huo yalikuwa katika halmashauri 119 ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau wameweza kudhibiti ugonjwa huo katika halmashauri 112 kati 119 na kubakiwa na halmashauri saba.

“Mkoa wa Dar es Salaam, halmashauri zote za Kigamboni na Ubungo,Temeke na halmashauri ya jiji hazina maambukizi mapya ya ugonjwa huu baada ya kusitisha umezeshaji wa kinga tiba na kubaki na kata 10 za Halmashauri ya Kinondoni ambazo zinamaambukiza mapya kwa asilimia 2.3.

“Kutokana na matokeo haya Wizara ya Afya inapenda kutoa taarifa rasmi kwa wananchi wa mkoa huu tunasitisha kampeni za uwezeshaji wa kingatiba ya ugonjwa lakini pia nitoe rai kwa wananchi kuchukua taadhari kwa kufanya usafi na kuua mazalia wa mbu,” amesema Ummy.

Amesema zoezi la umezeshaji kingatiba unafanywa kwa kata 10 za Manispaa ya Kinondoni ambazo ni Tandale,Kijitonyama,Mwananyamala,Kigogo,Mzimuni,Magomeni,Ndugumbi,Hananasifu, Kinondoni na Makumbusho.

Ummy ametoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kushiriki kampeni hiyo ya kingatiba zitakazoendelea kufanyika kwenye maeneo yao ili kuweza kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo.

Pia amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono jitihada za kutokomeza magonjwa yaliyokuwa ayapewi kipaumbele.

“Kupitia mkutano wa ‘Reaching the last mile’uliofanyika Desemba 2023 huko Dubai Rais aliahidi kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani milioni tatu katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2024 ili kufanikisha kutokomeza magonjwa haya hususani Matende na Mabusha,”amesema.

Ametaja Halmashauri zenye maambukizi mapya hivi sasa ni Pangani, Mafia, Kinondoni, Kilwa, Lindi Manispaa, Mtama na Mtwara Mikinfani ambako kuna jumla ya wakazi 1,203,359.

Kwa upande wake wake Mratibu wa Udhibiti wa Ugonjwa wa Matende na Busha Wizara ya Afya, Dk. Faraja Lyamuya amesema sababu zinazo changia maambukizi mapya katika baadhi ya maeneo ni jamii kutokuwa na uelewa wa kutosha pamoja na kuhamahama hatua inayosababisha kutoshiriki kikamilifu katika umezaji wa kingatiba

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles