30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Julio kocha mkuu Singida

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Siku chache baada ya kuvunja benchi lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na Thabo Senong, uongozi wa Singida Fountain Gate umemtambulisha Jamhuri Kiwelu kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho hadi mwisho wa msimu huu.

Timu hiyo imekuwa na matokeo yasiyoridhisha tangu baadhi ya wachezaji wake kutimkia Ihefu FC kipindi cha dirisha dogo kwa kupokea vichapo mfululizo.

Mchezo uliopita timu hiyo imepokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba, Uwanja wa Azam Complex, kabla ya hapo ilitoka kufungwa na Mtibwa Sugar 2-0, CCM Kirumba, Mwanza.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Rais wa Klabu ya Singida Fountain Gate, Japhet Makau, amesema mabadiliko hayo ni baada ya kubaini  upungufu kwenye benchi la ufundi, hivyo anaamini wanakwenda kuimarika sasa.

“Kocha mkuu anakuwa Julio akisaidiana na Ngawina Ngawina, pia tumemrudisha nyumbani Bartez (Ali Mustapha kocha wa makipa), tunaamini chini ya benchi hili tunakwenda kuimarika na tunaanza na mechi inayofuata dhidi ya Namungo, naamini mambo yatakuwa mazuri,” amesema Makau.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles