23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Maalim : Tumechoka kuporwa ushindi

Na MAUWA MOHAMMED – UNGUJA KASKAZINI

MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazaleando, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa anaamini Rais Dk. John Magufuli, atahakikisha uchaguzi unakuwa wa huru na haki kwani Wazanzibari wamechoka kuporwa ushindi wao.

Kauli hiyo alitoa jana Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B katika muendelezo wa ziara yake ya kichama inayoendelea katika Kisiwa cha Unguja.

“Naamini Rais Magufuli atahakikisha kilio cha Wazanzibari kinasikilizwa kwani wamechoka kuekewa kiongozi wasiyemchagua kuongoza nchi yao,”alisema Maalim Seif.

Kutokana na hali hiyo alimshauri Rais Magufuli kutenda uadilifu kwani wananchi wamechoka kudhulumiwa haki zao hasa kuputia uchaguzi.

“Wazanzibari wamechoka wapo tayari kupokea mabadiliko hakuna lisilowezekana kama wataamua,”alisema Maalim Seif 

Aidha alisema kuna njama nyingi  zitakazosababisha uchaguzi kutokuwa huru na wa haki kwani kwa upande wa Zanzibar Tume ya ZEC kwa kushirikiana na ofisi ya usajili wa matukio ya kijamii imewakosesha watu wengi kupata haki yao ya  vitambulisho.

Alisema kuwa ZEC na Ofisi ya Usajili wa Matukio ya Kijamii inafanya kazi kwa pamoja kwani wanajua kuwa watu hawapewi vitambulisho lakini imenyamaza kimya.

Baadhi ya vitambulisho vinatolewa kwa uficho lengo ni kumnyima fursa mwananchi jambo ambalo kwa sasa haliwezekani kwani Wazanzibari wanataka mabadiliko.

“Tume inajua wazi ukikosa kitambulisho cha mkazi huwezi kuandikishwa katika daftari la kupigia kura na maelfu ya watu wamekosa vitambulisho na vitambulisho vyengine wamepewa masheha ili kuwapatia watu na wamekuwa wakivitoa kwa ubaguzi,”alisema Maalim Seif.

Hata hivyo Maalim Seif alitupia lawama serikali na kudai kuwa yote yanayotokea ni kwa sababu  imekosa uadilifu na hivyo haiwezi kutenda jambo likawa lahalali.

Hivyo amezitaka vyombo vya Tume na Ofisi ya Msajili wa matukio  kufanya uadilifu ili wananchi waweze kujenga imani na vyombo hivyo.

Ziara hiyo ya kichama ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Malim Seif Sharif Hamad ni muendelezo wa ziara aliyoianza Pemba Juni 29, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles