26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Lusinde awavaa viongozi wa vyama 10 vya upinzani

ANDREW MSECHU-DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM) amedai vyama 10 vya siasa vilivyotoa tamko la kupinga muswada marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa  havina ajenda wala sera, hivyo hatua hiyo itachochea kupitishwa haraka  muswada huo.

Akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO),   Dar esSalaam jana, Lusinde alisema hatua ya vyama hivyo kuanza kupinga muswada huo inaibua hoja ya kuwataka wabunge kuanza kupingana navyo na hivyo kuufanya upitekwa ulaini utakapofika bungeni.

“Vyama hivi vya siasa lazima vitungiwe sheria zitakazowasimamia kwa sababu karibu vyote vinaonekana vinatumiwa na mabeberu. Kwanzahavina sera wala ajenda,” alisema.

Lusinde ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), alidai  hatua ya vyama hivyo kupinga muswada huo ni ‘kuunajisi’ suala ambalo hawawezi kukubaliana nalo.

Akisoma vipengele vya tamko hilo lililotolewa na vyama 10 vya siasa vya upinzani siku 10 zilizopita kisha kujibu kimoja baada ya kingine, alidai  anaona sasa weledi wa vyama vya siasa umeshuka.

Alisema kutokana na hali ilivyo katika vyama suala la kumpa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kama inavyopendekezwa katika muswada huo ni muhimu ili kusimamia vyama hivyo kwa sheria tofauti na ilivyo sasa ambako hanamamlaka yoyote ya sheria.

“Vyama hivi vinaelekeza nguvu kuilaumu serikali hii kuhusu muswada huo.

“Katika dini ya Uislamu kuna hadithi inayomhusu Izrailimtoa roho, kwamba anaona raha sana kutoa roho za wengine, ila ikifika siku yake kutolewa roho itakuwa kazi ngumu sana. Sasa kama Izraili ni zamu yetu,”alisema.

Lusinde pia alizungumzia suala la vyama hivyo kupinga kifungu kinachozuia vyama kufanya harakati akisema anashangaa hata Chadema wanaunga mkono suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles