29.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

LUPITA: WEINSTEIN ALITAKA KUNIFANYIA KITU KIBAYA

NEW YORK, MAREKANI


MSHINDI wa tuzo za Oscar nchini Marekani, Lupita Nyong’o, amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema kuwa alitakiwa kufanyiwa kitu kibaya na prodyuza wa filamu nchini humo, Harvey Weinstein.

Mrembo huyo raia wa nchini Kenya, aliyaelezea maisha yake ya safari ya filamu na kusema kuwa amekutana na changamoto mbalimbali hasa katika rushwa ya ngono.

“Nakumbuka wakati naanza kufanya vizuri kwenye filamu nilikuwa nakutana mara kwa mara na prodyuza Weinstein, kuna siku aliniomba kwenda kwake ili kuziangalia kazi zake, lakini nilishangaa baada ya kufika kwake akanilazimisha niingie chumbani kwake.

“Kitendo hicho kilinifanya nichukie sana na nilikuwa mkali japokuwa sikupiga kelele na bila ya kufanya hivyo nadhani angenifanyia kitu kibaya, ila nashukuru nilitoka salama,” alisema Lupita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles