31.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

ABE APATA USHINDI WA KISHINDO JAPAN

TOKYO, JAPAN


WAZIRI Mkuu wa Japan, Shinzo Abe ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa mapema, ambao umempatia mamlaka inayoimarisha msimamo wake mkali dhidi ya Korea Kaskazini.

Chama chake cha kihafidhina cha Liberal Democratic (LDP kilipata ushindi wa viti 311 katika Bunge  lenye  viti 465, kwa  mujibu wa matokeo  ya  awali.

Ushindi huo utamfanya Abe kuwa kiongozi  aliyekaa madarakani  muda mrefu zaidi nchini hapa.

Aidha ushindi  huo bila  shaka  utaongezea nguvu dhamira ya Abe kupambana na hatari  ya nyuklia inayoletwa na  Korea Kaskazini.

Mamilioni  ya Wajapan  walijitokeza  kupiga  kura licha  ya  mvua kubwa  na  upepo  mkali, wakati kimbunga  kiliposhambulia  taifa hilo.

Wengi walipiga kura zao mapema  baada  ya  kutolewa tahadhari ya kimbunga  hicho.

“Naunga  mkono  msimamo  wa  Abe  katika  kuipa  Korea  Kaskazini mbinyo,” alisema  mpiga  kura  mmoja, Yoshihisa Lemori, wakati akipiga  kura  yake  huku  mvua  kubwa  ikinyesha  mjini  Tokyo.

Hata hivyo, LDP imefaidika  kutokana  na  upinzani  dhaifu na uliogawika huku vyama  vikuu  viwili vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo  vikiwa vimeundwa  wiki  kadhaa  tu  zilizopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles