32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Lupita Nyong’o na rundo la vipaji

Lupita Nyong’o
Lupita Nyong’o

Na BADI MCHOMOLO,

UKIZUNGUMZIA wasanii wa filamu Afrika ambao wanafanya vizuri katika tuzo kubwa duniani hauwezi kumuacha Lupita Nyong’o ambaye anatokea nchini Kenya.

Kwa sasa msanii huyo makazi yake ni nchini Marekani, anatangaza vizuri Afrika katika tuzo mbalimbali barani Ulaya kama vile Tuzo za Oscar na Black Entertainment Television (BET).

Kwa sasa msanii huyo anatamba kutokana na filamu mpya inayojulikana kwa jina la Queen of Katwe na The Jungle Book, lakini awali alikuwa anatamba na filamu ya 12 Years a Slave ambayo ilitoka mwaka 2013.

Katika filamu hii ya Queen of Katwe ambayo trailer yake imeachiwa tangu Septemba 23, mwaka huu, imegharimu kiasi cha Dola milioni 15 za Kimarekani.

Filamu hiyo inaonesha maisha ya mwanamke wa nchini Uganda ambaye anatokea katika maisha ya hali ya chini lakini anapambana kwa ajili ya kuikomboa familia yake na taifa kwa ujumla.

Filamu hiyo ni habari ya mjini kwa sasa nchini Uganda kwa kuwa sehemu kubwa iliyotumika katika kucheza filamu hiyo ni nchini Uganda na imekuwa ikizungumziwa sana na idadi kubwa ya mashabiki barani Afrika.

Katika filamu hiyo Lupita ameonesha uwezo wake na kufanya filamu kuwa na mvuto wa aina yake na inaweza kumpa nafasi nyingine ya kufanya vizuri kwenye tuzo mbalimbali.

Hata hivyo msanii huyo amedai kuwa anajivunia kuwa mtu kutoka Bara la Afrika kwa kuwa anaweza kulitangaza vizuri bara hilo.

Mbali na kufanya vizuri katika filamu, lakini msanii huyo amejigundua kuwa ana kipaji cha kuimba muziki, lakini amedai kuwa hawezi kufanya kama sehemu ya kazi yake.

Lupita amedai kuwa kuna wakati anakuwa ametulia na kufikiria jambo la kufanya na ndipo anajikuta akiandika mistari na kuanza kuimba.

Akiwa katika mapumziko baada ya kuachiwa kwa filamu hiyo mpya ya Queen of Katwe, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 33, alipanga kufanya sherehe kwa ajili ya kufurahia kufikisha marafiki milioni tatu  kwenye akaunti yake ya Instagram.

Aliamua kurekodi video fupi akiwa anaimba wimbo wa kuwashukuru marafiki kwenye akaunti hiyo ya Instagram.

Katika baadhi ya mistari ambayo imeimbwa na msanii huyo akiwa na furaha kubwa, inasema: “Nimezaliwa nchini Mexican, mishipa yangu ya damu imekulia nchini Kenya, huku nikiwa na rangi ya chocolate, lakini kwa sasa nafanya vizuri ulimwenguni.”

Hata hivyo msanii huyo amedai kwamba ana uwezo wa kufanya vizuri katika muziki kama akiamua kuutolea macho na amedai kuwa kama ataamua kufanya hivyo basi wanaweza kumuita Trouble Maker.

Msanii huyo ameweka wazi kuwa katika filamu ambayo imemfanya awe na jina kubwa ni ile ya 12 Years a Slave, ambayo imemfanya apate jumla ya tuzo nane.

“Ninaamini filamu ni sehemu ya maisha yangu na ndiyo maana leo nipo hapa, naweza kufanya muziki lakini sina mpango wa kufanya hivyo labda iwe kama sehemu ya starehe yangu.

“12 Years a Slave imenifanya niwe hapa kwa sasa, hivyo akili yangu kila siku ni kuzidi kufanya makubwa zaidi ya filamu hiyo, ninaamini ninaweza kufanya hivyo kwa kuwa uwezo wa kufanya hivyo ninao,” anasema Lupita.

Msanii huyo anatarajia kuonekana tena katika filamu mpya ambayo itaachiwa Desemba 15, mwakani ikijulikana kwa jina la Star Wars, Episode VIII.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles