21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

LUKUVI ATUA NA MWAROBAINI WA MIGOGORO YA ARDHI LINDI

Hadija Omary, Lindi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema amekuja Lindi na majibu ya utatuzi wa Mgogoro wa mpaka wa kijiji cha Nanjilinji A na Kijiji cha Mirui.

Lukuvi ameyasema hayo jana kabla ya kuanza kikao kilichowakutanisha wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya za Kilwa na Liwale.

“Baada ya timu ya wataalamu kupitia nyaraka mbalimbali zilizotumika katika uanzishwaji wa wilaya na vijiji hivyo ambapo licha ya kutatua mgogoro huo, wizara kwa kushirikiana na mkoa na wilaya watapima na kuweka alama za kudumu (mawe) za mipaka katika vijiji hivyo ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea mpango wa matumizi bora ya ardhi,” amesema Lukuvi.

Pamoja na mambo mengine, Lukuvi pia amesema wizara yake imejipanga kuhakikisha inaboresha ofisi zake za kanda ambapo kwa Kanda ya Kusini maofisa wote muhimu wameshaagiziwa vifaa vya kazi na vitawasili mwezi ujao ili kuhakikisha shughuli nyingi zinazohusu masuala ya ardhi zinamalizika katika Ofisi za Kanda na si wizarani kama ilivyokuwa awali.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akimkaribisha Waziri Lukuvi amesema mkoa unaendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo.

Alitaja baadhi ya migogoro hiyo kuwa ni wananchi kuvamia shamba la Mahumbika, Shamba la Mkwaya katika Wilaya ya Lindi, mgogoro wa mpaka kati ya wananchi na Kikosi Namba 843 cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Kikosi 41cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vilivyopo Wilaya ya Nachingwea

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles