24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Luis, Kahata wazua hofu

Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

KIWANGO cha juu kinachoonyeshwa na viungo wa Simba, Luis Miquissone, Francis Kahata, Hassan Dilunga na wengineo, kimezua hofu miongoni mwa timu pinzani za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kahata, Dilunga, Clatous Chama wamekuwa muhimili wa Simba katika eneo la kiungo, wakiwa chachu ya mabao ya timu hiyo, huku Luis alionyesha si mtu wa mchezo mchezo.

Wachezaji hao pamoja na ‘mkongwe’ Jonas Mkude, wametengeneza muunganiko mzuri unaoifanya Simba kuwa moto wa kuotea mbali.

Ukiachana na uwezo wao wa kupora mipira, kupiga pasi na kuiwezesha timu yao kutawala mchezo, pia viungo hao wamekuwa wakifunga mabao ama kuwatengenezea nafasi washambuliaji wao, Meddie Kagere na John Bocco.

Kiwango cha nyota hao, kimeonekana kuwagusa makocha wa timu nyingi, akiwamo wa Kagera Sugar, Mecky Mexime ambaye alikiri Wekundu wa Msimbazi hao wanatisha zaidi katika safu ya kiungo.

Kocha mwingine ambaye ameonekana kupatwa na hofu juu ya cheche za viungo hao wa Simba, ni Francis Baraza wa Biashara United.

Baraza aliliambia MTANZANIA jana kuwa siku zote alizoshuhudia mechi za Simba, roho yao ipo katika eneo la kiungo, hivyo anatakiwa kuwa makini nayo kuelekea mechi ya kesho ya Ligi Kuu Tanzania Bara, watakayokutana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Alisema katika mchezo huo, ataingia kwa nidhamu ya hali ya juu kwa sababu anajua ubora wa Wanamsimbazi hao ulipo.

“Simba ubora wake ni eneo la kiungo, tunafanya maandalizi tukijua ni wapi tunatakiwa kuwa makini napo, sio kama naogopa, ila inafahamika mpinzani wako akiwa bora ujipange vipi.

“Wachezaji wangu nimekaa nao, nimewaambia hali halisi na wenyewe wameshuhudia mechi za Simba, wanajua nini cha kufanya, kikubwa ni kuzingatia nidhamu,” alisema Baraza.

Alifafanua kuwa katika mchezo huo, ataingia na mbinu mbadala kuhakikisha wanapambana hadi dakika ya mwisho, wakiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles