28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Molinga avujishiwa siri nzito

Na ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba na Yanga, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’,  anaamini nyota wa Wanajangwani, David Molinga, anaweza kumpita kinara wa mabao Ligi Kuu Tanzania Bara, Meddie Kagere, lakini iwapo atakuwa mtulivu anapokuwa mbele ya lango.

Kagere ndiye anayeongoza orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara, akiwa na mabao 13, wakati Molinga ana saba.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mmachinga aliyeweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo kwa kucheka na nyavu mara 26 msimu wa 1999, alisema kinachomponza Molinga ni pupa.

“Molinga anashindwa kutulia akiwa ndani ya 18 au eneo ambalo anaweza kuipa Yanga mabao, endapo ataamua kuyafanyia kazi makosa anayoyafanya akiwa kwenye eneo sahihi la kufunga, hadi mwisho wa msimu anaweza kuwa na idadi kubwa ya mabao.

“Sio kuipa tu Yanga mabao mengi, bali pia kuwa mfungaji bora mwaka huu kwa sababu tofauti ya mabao kati yake na Kagere sio kubwa sana, anaweza kumfikia kwenye michezo mitatu au minne kama ataamua,” alisema Mmachinga.

Pamoja na kuzichezea Simba na Yanga, Mmachinga alipata umaarufu zaidi akiwa na kikosi cha Wanajangwani kutokana na cheche zake, zaidi ikiwa ni uwezo wake wa hali ya juu wa kufunga mabao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles