31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Lugola awataka polisi kutoa dhamana hadi wikiendi

           Felix Mwagara, Kasulu



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari Polisi kutoza fedha kwa ajili ya dhamana kwa watuhumiwa waliopo mahabusu katika vituo vya polisi nchini.

Aidha, amesema dhamana hizo zinapaswa kutolewa saa 24 katika siku zote za wiki na si vinginevyo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwamo siku za mapumziko.

Lugola amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Basanza wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, na uongeza kuwa ni marufuku kwa askari yeyote atakayeshindwa kutoa dhamana kwa kosa ambalo lina dhamana.

“Hii tabia sijui imetoka wapi ambayo imejengeka kwa baadhi ya askari polisi, eti mtu akiingia mahabusu ya polisi Ijumaa ikifika Jumamosi na Jumapili hawatoi dhamana wakisema dhamana hadi Jumatatu, hii tabia si sahihi na ife haraka iwezekananavyo,” amesema Lugola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles