29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

WALIMU SABA WAFUKUZWA KAZI KWA UTORO IGUNGA

Na ABDALLAH AMIRI-IGUNGA


WALIMU saba   katika shule mbalimbali za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wamefukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwamo  utoro kazini.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  juzi, Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wilaya ya Igunga, Hamisi Mpume, aliwataja walimu hao kuwa ni Paul Msabila aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Igunga mjini, Mary Elvance Kesi aliyekuwa akifundisha Shule ya Msingi Bulunde.

Wengine ni Lazaro Cheyo wa Shule ya Sekondari Nguvumoja, Leonard Chakupewa wa Shule ya Msingi Ziba, Rogasian Pacho wa Shule ya Msingi Nyandekwa, Sostenes  Chiboko wa Shule ya Sekondari ya Sungwizi   na Faustine Obadia wa Shule ya Msingi Ziba.

Alisema walimu hao walifikishwa katika tume ya utumishi wa walimu ya Wilaya ya Igunga na kubainika kuwa na makosa mbalimbali yakiwamo utovu wa nidhamu na utoro kazini kwa muda mrefu pasipo taarifa yoyote kwa mwajiri wao.

Mpume alisema pia wapo baadhi ya walimu ambao hakuweza kuwataja majina ingawa ameshapewa barua za onyo baada yakubaini makosa yao siyo yakufukuzwa kazi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, ambaye pia ni Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Ntulila Hadoni,  alisistiza taratibu zote za utumishi zimezingatiwa kabla ya kuchukuliwa uamuzi huo kwa mujibu wa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles