24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 30, 2023

Contact us: [email protected]

Liverpool imetakiwa kutoa pauni 50 kama inamtaka Teixeira

AlexTeixeiraLIVERPOOL, England

MSHAMBULIAJI wa Shakhtar Donetsk, Alex Teixeira, yupo tayari kuhamia Anfield, ingawa klabu yake inaonekana kutokuwa tayari kumuachia nyota huyo katikati ya msimu.

Mtendaji Mkuu wa Donetsk, Sergei Palkin, alisema Liverpool inatakiwa kulipa pauni milioni 50 ili kupata huduma ya Mbrazil Teixeira.

Hatua hiyo inakuja huku mchezaji mwenyewe akithibitisha kwamba anapenda kujiunga na klabu ya Liverpool haraka iwezekanavyo.

Liverpool dau lao la pauni milioni 24 lilipigwa chini na klabu ya Shakhtar, ambayo ilidaiwa kumhitaji mchezaji huyo kwenye michuano ya ligi ya Europa.

Palkin alisisitiza kwamba walikataa dau la pauni milioni 32 pamoja na ziada ya pauni milioni 4, kutoka klabu ya Liverpool.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,282FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles