28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Alaba ana furaha kuwa Bayern Munich

alabaMUNICH, Ujerumani

BEKI wa klabu ya soka ya Bayern Munich, David Alaba, amesema ana furaha kuwa katika klabu hiyo na kudai kwamba anafahamu kwanini wachezaji wanataka kwenda kucheza katika Ligi Kuu England.

Alaba alisema kwamba hana haraka ya kukaribisha mazungumzo mapya na klabu yake na kudai kwamba anatambua Ligi Kuu England ni miongoni mwa ligi bora duniani.

Hata hivyo, Thomas Muller, Jerome Boeteng pamoja na Javi Martinez wameongeza mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo, huku ikiamini kwamba Alaba atakubali kusaini mkataba mpya muda mfupi ujao.

Ingawa inadaiwa kwamba Alaba alidai kwamba hafikirii juu ya kuwa na mkataba wa muda mrefu na huenda akaondoka katika klabu hiyo.

“Mkataba wangu unakwisha mwaka 2018, nilipata majeraha ya muda mrefu, hivyo wakati wote nilifikiria juu ya kurejea katika kiwango changu, sikuwahi kufikiri juu ya mkataba katika akili yangu,” alisema Alaba, alipokuwa akizungumza na kituo cha redio AZ cha nchini Ujerumani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles