25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

LISSU AKAMATWA TENA DODOMA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema), huku likidai sababu za kumkamata ni maagizo kutoka makao makuu ya jeshi hilo Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana kwa simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo, huku akidai sababu za kumkamata hazijui kwa sasa ila wao wametekeleza agizo la kutoka makao makuu ya jeshi.

Alisema walimkamata mbunge huyo saa 11 jioni akiwa katika viwanja vya Bunge alipokuwa akihudhuria vikao.

“Ni kweli tumemkamata majira ya saa 11 jioni leo (jana) na mimi narejea Dodoma, nilikuwa Dar es Salaam. Sababu za kumkamata ni ana makosa anatakiwa akajibu Dar es Salaam na mimi siwezi kukwambia sababu wao ndio wana sababu na wanajua kwanini walituelekeza tumkamate,’’ alisema.

Kamanda Mambosasa alisema yeye alifuata maagizo aliyoelekezwa ndiyo maana akaagiza akamatwe mbunge huyo.

“Sina cha kukwambia zaidi ya kukwambia sijui sababu za kukamatwa kwake,’’ alisema.

Hii ni mara ya tatu kwa mbunge huyo kukamatwa.

Kwa mara ya kwanza alikamatwa akidaiwa kufanya mkutano kinyume cha sheria jimboni kwake na mara ya pili alidaiwa kutamka maneno yenye utata dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles